Wednesday, February 24, 2016

Timu ya Yanga imekuwa ya kwanza kufuzu kucheza robo fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cu (ASFC) baada ya kuichapa JKT Mlale ya Ruvuma kwa bao 2-1 kwenye uwanja wa taifa.
Mlale ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 22 kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji Shabani Mgandila aliyefunga goli hilo kwa uwezo mkubwa baada ya safu ya ulinzi ya Yanga kufanya makosa.
Yanga ilikuja juu na kusawazisha bao hilo mfungaji akiwa ni Paul Nonga aliyeunganisha pasi ya Geofrey Mwashiuya dakika ya 38 kipindi cha kwanza.
Thaban Kamusoko akitokea benchi kuchukua nafasi ya Salum Telela aliipa Yanga ushindi dakika ya 58 kipindi cha pili baada ya kuunganisha pasi ya Mwashiuya ambaye leo alikuwa kwenye kiwango kizuri na kufanikiwa kupika mabao yote ya Yanga.
Yanga imeutumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi kuelekea mechi ya Jumamosi ya klabu bingwa Afrika mchezo wa marudiano dhidi ya klabu ya Cercle de Joachim ya Mauritius.
Hans aliwaanzisha wachezaji wengi wa benchi kwenye mchezo ili kutoa nafasi kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza kupata mapumziko lakini pia aliwatumia nyota kadhaa wa kikosi cha kwanza ambao walikosa michezo kadhaa kutokana na majeruhi pamoja na kutumikia kadi.
Cannavaro alicheza dakika zote 90 za mchezo huo akitokea majeruhi, Yondani aliyekuwa akitumikia kadi nyekundu alianza na kumaliza sambamba na Cannavaro. Donald Ngoma na Thabani Kamusoko waliingia kipindi cha pili kuipa tafu Yanga iliyokuwa sare kwa bao 1-1 na Mlale.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video