Kocha wa Arsenal Arsene Wenger ametoa pongezi kwa safu ya ushambuliaji ya Barcelona inayoongozwa na utatu wa Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar, lakini amesisitiza kwamba atatafuta namna ya kupambana na wakali hao.
The Gunners kesho watapambana na Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa barani Ulaya huku wakiwa na historia mbaya mbele ya Wakatalunya hao, wakishinda mara moja kati ya michezo saba waliyokutana.
“Ni safu inayotisha sana," Wenger aliwaambia wanahabari. "Naamini kwamba mbali na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja walionao Messi, Suarez na Neymar, wana uelewano mkubwa sana.
“Nimeona Cristiano Ronaldo akisema kwamba Messi alimpasia mpira wa penati Suarez wiki iliyopita ili awe juu katika kinyang'anyiro cha ufungaji bora.
“Unapoona mtu kama Messi, ambaye anaweza kufunga goli lake la 300, halafu anampa pasi Suarez wakati hiyo ndiyo fursa yake ya kufunga goli la 300, maana yake kuna kitu cha kipekee kati yao."
“Inaonekana kana kwamba wakati wote ni furaha kwao [MSN] kulinga na wanavyocheza. Hawaonekani kama wanacheza chini ya presha yoyote ile kwa sababu kila wakatio ni mwepesi kwao”,
0 comments:
Post a Comment