Thursday, February 11, 2016

Kwa sasa hivi moja ya habari kubwa zinazozungumziwa sana ni kuhusu Jose Mouriho kujiunga na club ya Manchester united baada ya msimu huu kuisha. Kocha yoyote akiingia kwenye kikosi kipya kuna uwezekano mkubwa wa yeye kutaka kufanya mabadiriko ya kikosi hicho. Kama Jose akitaka kubadirisha kikosi cha United basi hawa ni wachezaji 10 ambao anaweza kuwafikiria kwenye nafasi mbalimbali za kikosi cha Manchester united.

Edinson Cavani:
Striker wa Uruguay inaripotiwa kwamba hana furaha ndani ya PSG kwasababu Zlatan Ibrahimovic anacheza sana kwenye nafasi yake na anaonekana kuwa kinara wa club. Kama Jose akitoa ofa kwa ajili ya Cavani kuja Manchester basi kuna uwezekano wa kumpata.

Harry Kane:
Jose alitaka kumsajili huyu mchezaji ndani ya Chelsea akitokea Tottenham mwezi wa kwanza lakini ikashindikana. Kuna uwezekano kwamba Jose anaweza kutoa ofa mpya kwa ajili ya mchezaji huyu.

RAPHAEL VARANE
Huyu jamaa alikua na uhusiano mzuri sana na Jose wakati yupo Real Madrid. Beki huyu pia yupo kwenye uwezekano mkubwa wa kuungana na bosi wake wa zamani na kusaidia kwenye sehemu ya ulinzi.

RUBEN NEVES
Kutokana na ripoti ni kamba Manchester wanataka sana kumsajili midfielder huyu kwa ajili ya club yao. Kwasababu Jose ni raia wa Portugal na mchezaji huyu pia ni wa Portugal, kuna uwezekano mkubwa kujuana kwa wawili hawa kukafanikisha dili hili.

WESLEY SNEIJDER
Mchezaji huyu wa Ga;atasaray alikua na uhusiano mzuri na kocha wake Jose wakati wapo Inter Milan. Mara moja Sneider aliwai kumuita Mourihno kama kocha bora dunia nzima, labda Jose anaweza kucheza kamali ya uzoefu wa Sneijder na kumleta Manchester United.

JOHN STONES
Mourihno alikua na hamu kubwa ya kumsajili mchezaji huyu mchanga kutoka Everton wakati yupo Chelsea lakini mambo hayakwenda kama alivyopanga. Sasa kwa nguvu ya United na hamu ya Jose kuwa na John Stones labda atafanikiwa akijaribu.


SEAMUS COLEMAN
Mchezaji wa Everton amekua target ya muda mrefu ya Mancheter United ili kuongeza nguvu. Aina hii ya wachezaji ndio ambao Jose anawapenda, labda atafanikiwa kumleta kama akijaribu.

ANTOINE GRIEZMANN
Star wa Atletico Madrid alikua anatajwA sana kuhamia Chelsea wakati Mourihno alivyokua manager, tunategemea Jose anaweza kujaribu kumsajili akiwa Manager wa Chelsea.


LOIC REMY
Striker awa Ufaransa mara kadhaa alikua akimtetea kocha wake Mourihno wakati yupo Chelsea, kama Jose akiwa na shida nae anaweza kutoa ofa na Remy sio rahisi kukataa kutokana na uhusiano wao mzuri.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video