Wednesday, February 24, 2016

Historia bado imeendelea kuitafuna Azam FC kwenye uwanja wa Sokoine baada ya kulazimishwa sare ya bil kufungana dhidi ya wenyeji wa mchezo huo Tanzania Prisons ‘wajelajela’.
Azam haijawahi kushinda mbele ya Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Sokoine tangu timu hizo zilipoanza kukutana. Mchezo huo umekuja baada ya Azam kutoa kichapo cha bao 3-0 kwa Mbeya City Jumamosi iliyopita kwenye uwanja huohuo wa Sokoine.
Mchezo wa leo ulikuwa ni wa 12 ukizikutanisha Tanzania Prisons dhidi ya Azam kwenye ligi kuu ya Vaodacom Tanzania bara.

Rekodi
Azam FC imefanikiwa kushinda mechi tatu (3) lakini mechi zote hizo imeshinda ikiwa kwenye uwanja wake wa Azam Complex huku ikiwa haijawahi kupata ushindi mbele ya Prisons ikiwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Tanzania Prisons pia imeshinda michezo mitatu dhidi ya Azam FC, miwili kati ya hiyo imeshinda ikiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Sokoine, Mbeya huku ikiwa imetoka sare kwenye michezo mitatu.
Timu zote zimetoka sare mara sita kati ya michezo 11 waliyokutana kwenye ligi tangu Azam ilipopanda kucheza ligi kuu ya Tanzania, michezo sita iliyobaki kila timu imeshinda michezo mitatu.

Ratiba ya mechi za timu hizo kwenye ligi

Azam FC
March 5, 2016 Azam itakuwa mwenyeji wa Yanga kwenye mchezo wa ligi utakaopigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam huku timu hizo zikiwa zinalingana kwa pointi (45) lakini Yanga ikiwa kileleni mwa lgi kwa tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga.

Tanzani Prisons
Tanzania Prisons watakuwa nyumbani tena kuikaribisha Stand United kwenye uwanja wao wa nyumbani Sokoine March 5, 2016. Prisons imefikisha pointi 32 baada kucheza mechi 20 pointi sawa na Mwadui FC na inaendelea kusalia katika nafasi ya sita.
Msimamo wa ligi baada ya mchezo wa Tanzania Prisons vs Azam (nafasi nane za juu)

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video