Louis van Gaal amedai kuwa ni muhimu kwa meneja ajaye wa Manchester United kuonesha imani kubwa kwa wachezaji vijana, vinginevyo atapata wakati mgumu sana kunako dimba la Old Trafford.
Mdachi huyo anatarajiwa kutimka klabuni hapo Juni, 2017 pindi mkataba wake utakapofikia kikomo, japokuwa mustakabali wake kwa sasa upo tenege kutokana na mwenendo usioridhisha wa klabu hiyo.
Van Gaal amejitahidi kuweka imani yake kubwa kwa vijana msimu huu, kama vile Cameron Borthwick-Jackson na Jesse Lingard bila kusahau Anthony Martial ambaye amenunuliwa kutoka Monaco.
"Nadhani watu wakiwa wanawaona hawa vijana, watakuwa wakinikumba kutokana na ukweli kwamba, huu ni urithi pekee, lakini kamwe hamuwezi kuwaambia," alisema.
"Ni muhimu sana kwa kocha ajaye kuonesha imani kwa wachezaji vijana. Lakini maneno yangu si sheria.
"Kama baada ya kustaafu hapa, United wataajiri kocha ambaye hatakuwa na imani kwa wachezaji vijana, kutakuwa na wakati mgumu sana.
"Muhimu pia kwa bodi ya klabu kuangalia uwezo wa kocha ambaye atakuja kushika hatamu hapa.
"Kama wataniuliza kocha ambaye ningependa aje baada yangu, nitawaambia, lakini baada ya hapo, uamuzi utabaki kwao.
0 comments:
Post a Comment