Louis van Gaal amemwambia Paul Scholes ajaribu kuwa na maoni chanya kuhusu klabu ya Manchester United, lakini akisisitiza kwamba kamwe hatamwambia Ryan Giggs azungumze chochote juu ya maoni yanayotolewa na nguli huyo wa zamani wa Man United.
Mwanzoni kabisa mwa mzunguko wa pili, United ilikubwa na jinamizi la kutoshinda mara baada ya kucheza michezo kadhaa bila ya kushinda hata mmoja, hali iliyosababishwa kukoselewa na vyombo vya habari pamoja na mashabiki wao, huku Scholes akiwabwatukia Van Gaal na wachezaji wake kucheza mpira uliokosa mvuto.
Licha ya kupata matokeo mazuri na kuonesha kiwango bora kabisa hivi karibuni, bado kuna hali ya sintofahamu klabuni hapo juu ya kocha yupi atashika maikoba msimu ujao, huku jina la Mourinho likitajwa sana na vyombo vya habari mbalimbali nchini humo.
Van Gaal amesema kwamba kamwe hawezi kusababisha msaidizi wake, Giggs, kuwa mpuuzi kwa kumwambia amjibu Scholes ambaye ni mchezaji mweza wa zamani wa klabu hiyo na kusisitiza kuwa, maoni mengi yanayotolewa na Scholes yamejaa mtazamo hasi kwa klabu hiyo.
"Sifikirii kumpa msongo wa mawazo Ryan kutokana na urafiki mkubwa alionao na Scholes," alisema. "
"Halitakuwa jambo la msingi mimi kumwambia Giggs amjibu Scholes kwa anachokiongea juu ya Manchester United.
"Anachokizungumza Scholes ni muhimu afikirie kwanza. Kila binadamu ana haki ya kutoa mtazamo wake. Mimi siumizwi na hilo, nadhani ni kitu kizuri tu.
"Lakini tatizo langu mimi ni pale muda wote anapokuwa na mtazamo hasi juu ya mtu fulani, mimi nadhani anatakiwa kuwa na matazamo chanya walau kidogo."
0 comments:
Post a Comment