Thursday, February 25, 2016

Mwinyi Kazimoto
Wakati wengi walishangaa kwa nini kiungo Mwinyi Kazimoto alibadilishwa Jumamosi iliyopita wakati Simba ikiivaa Yanga, taarifa za uhakika zinasema, mwenyewe alikataa kuendelea.
Kazimoto alimuomba Kocha Jackson Mayanja kumuondoa kikosini kwa kuwa asingeweza kuendelea na mchezo huo ambao Simba walipoteza kwa mabao 2-0.
“Ni kweli, Kazimoto ndiye aliyeomba kutolewa. Alimwambia kocha asingeweza kuendelea ingawa hakusema sababu hasa ya msingi,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Kutokana na hali hiyo, Mayanja aliamua kumbadilisha na baadaye alifanya mabadiliko tena kwa kuwa tayari beki wake, Abdi Banda alikuwa amelambwa kadi nyekundu.
Simba ilianza vizuri mechi hiyo, lakini mabadiliko mfululizo pamoja na kadi nyekundu ya Banda vilionyesha kuwavuruga.
Yanga waliingia kipindi cha pili wakiwa na kasi zaidi na kuutumia vizuri mwanya wa Simba kuwa na kadi nyekundu kuimaliza kwa kupata bao la pili la Amissi Tambwe, lililomaliza kabisa mchezo.
Creidit:Salehjembe

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video