Legend wa Manchester United Paul Scholes anaamini kwamba klabu yake ya zamani itapata wakati mgumu sana wakati itakapokutana na Arsenal wikeindi hii katika mchuano wa Ligi Kuu nchini Uingereza.
United watakutana na Arsenal ambao wako nafasi ya tatu kwa sasa, huku wakiwa na ari kubwa baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 5-1 Midtjylland kwenye Ligi ya EUROPA.
Scholes amesema kwamba Arsenal wataingia wakiwa kama timu inayopewa nafasi kubwa zaidi licha ya matokeo mazuri ya United katika mechi za michuano mbalimbali iliyopata hivi karibuni.
“Arsenal ni timu nzuri ikiwa na wachezaji hatari sana kwenye safu ya ushambuliaji na kwa namna beki ya United ilivyo, ninapata hofu kubwa sana,” Scholes alisema.
“Kama ukiangalia kwa umakini safu ya ushambuaji ya Arsenal imejaa watu wenye kasi kubwa, hivyo itawawi vigumu sana United kuendana na kasi hiyo. Sote tunajua kwamba utakuwa ni mchezo mgumu sana.”
0 comments:
Post a Comment