
Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajiwa kuendelea leo na kesho katika mzunguko wa lala salama (raundi ya 9), kwa timu zote 24 kushuka dimbani pointi 3 muhimu katika msimamo ili kuweza kupanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Leo Kundi A, Green Warriors v Transit Camp (Mabatini), Singida United v Abajaro Tabora (Namfua), Mvuvumwa FC v Mirambo (Lake Tanganyika).
Kundi B, Jumapili Pamba FC v Madini FC (CCM Kirumba), AFC ARUSHA v Bulyanhulu (Sheikh Amri Abeid), huku Jumatatu Alliance School v JKT Rwamkoma (CCM Kirumba).
Jumamosi Kundi C, Cosmopolitan FC v Abajaro Dar (Karume), Jumapili Mshikamano FC v Kariakoo FC (Mabatini), Villa Squad v Changanyikeni (Karume).
Kundi D, Jumamosi African Wanderes v Mkamba Rangers (Wambi Mafinga), Jumapili Wenda FC v Sabasaba FC (Sokoine) huku Jumatatu The Mighty Elephant v Mbeya Warriors (Majimaji)
0 comments:
Post a Comment