Saturday, February 20, 2016

HII SIO TAARIFA NJEMA HATA KIDOGO KWA WANAYANGA
Baada ya hadithi za hapa na pale, hatimaye nahodha na beki wa kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ametangaza hatacheza mechi ya leo dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwani bado hayupo fiti.
Cannavaro alitegemewa kurejea uwanjani na kucheza mechi ya leo namba 153 ya Ligi Kuu Bara lakini pamoja na madaktari wa Yanga kujitahidi kumtibu jeraha la enka, kila kitu kimeshindikana. 
Cannavaro ambaye hakuwepo uwanjani tangu Novemba mwaka jana kutokana na jeraha hilo, alisema amefikia uamuzi huo wa kutocheza dhidi ya Simba kwa kuwa alishindwa kufanya mazoezi ya mwisho ya pamoja na wenzake.
“Nimejitoa rasmi katika mechi hii kwani nimeshindwa kufanya mazoezi ya mwisho kutokana na kutopona vizuri jeraha la enka, nahitaji wiki moja zaidi ili nipone zaidi.
“Nilitaka nicheze dhidi ya Simba kwani ni mechi ngumu sana na yenye hisia, nilitaka kuisaidia timu yangu lakini sitaweza kucheza kutokana na hali yangu,” alisema Cannavaro.
Kwa maana hiyo, Yanga sasa itawatumia Mbuyu Twite na Vincent Bossou katika beki ya kati leo dhidi ya Simba.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video