


Paris Saint Germain wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Chelsea katika pambano la Klabu Bingwa Ulaya hatua ya 16 bora lililopigwa kwenye dimba la Parc des Princes jijini Paris Ufaransa.
Magoli ya PSG yalifungwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 39 na Edinson Cavani dakika ya 78 huku bao la Chelsea likifungwa na John Mikel Obi dakika ya 45.
Video
Katika mchezo mwingine uliozikutanisha timu za Benfica na Zenit St. Petersburg, Benfica wamefanikiwaa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 nyumbani.
0 comments:
Post a Comment