Chelsea wamesafiri kuelekea Ufaransa wakiwa tayari kuanza kampeni yao ya kufuzu hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya wapinzani wao Paris Saint Germain ambao msimu uliopita waliwatupa nje.
Chelsea wameingia katika rekodi mbovu kabisa EPL baada ya kuanza na matokeo mabovu kuwahi kutokea kwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo, hali iliyopelekea kumtimua kocha wao Jose Mourinho na mikoba yake kuchukuliwa na Guus Hiddink.
ZLATAN IBRAHIMOVIC vs BRANISLAV IVANOVIC
Hawa ni wachezaji wawili wenye roho ngumu za Ki-Balkan, ambao mara nyingi si watu wenye uvumilivu bali wenye hasira kali za papo kwa hapo.
Ivanovic ataongoza safu ya ulinzi ya Chelsea kutokana na kukosekana kwa John Terry anayesumbuliwa na majeraha.


Ivanovic (kulia) na Zlatan Ibrahimovic.
Ibrahimovic, huyu mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu. Zlatan bado anatafuta kwa udu na uvumba taji la UEFA kutokana na kulikosa katika masiha yake yote ya soka.
Zlatan anatarajiwa kuwa na hasira kubwa kutokana na kile alichokiita ni upumbavu baada ya wachezaji wa Chelsea kumshawishi mwamuzi ampe kadi nyekundu kutokana na kumchezea madhambi Oscar wakati timu hizo zilipokutana katika hatua kama hii msimu uliopita. Aliwafananisha wachezaji wa Chelsea kama watoto wanaolia ‘cry babies’, hivyo hasira alizonazo ni ishara kuwa kutakuwa na battle ya maana kwa wachezaji hawa.
THIAGO SILVA vs DIEGO COSTA
Hatimaye Costa sasa amerudi kwenye ubora wake baada ya kuanza kuzifumania nyavu kwa kasi, matumaini makubwa ya Chelsea yamelalia mikononi mwake. Katika michezo 10 ya mwisho kwa Chelsea Costa amefunga magoli nane.


Diego Costa (kulia) ana kazi kubwa ya kufanya mbele ya Thiago Silva -beki bora wa kati kwa sasa
Thiago Silva, mlinzi mwenye asili ya Brazilian na nahodha wa PSG, watu wengi sana wanamtaja kama beki bora wa kati ulimwenguni, shughuli ayke na Costa kamwe haitakuwa ya kitoto kutokana na wawili hao kuwa katika ubora wa hali ya juu kwa sasa. Anasifika sana kwa kupanga vizuri safu yake ya ulinzi
ANGEL DI MARIA vs BABA RAHMAN
Licha ya kuwa hajakomaa vya kutosha, BabaRahman anaonekana kuwa msaada mkubwa kwa Chelsea kwa sasa kutokana na kukosekana kwa Kurt Zouma na John Terry. Baba Rahman anacheza kama beki wa kushoto, nafasi ambayo mara nyingi hucheza Cesar Azplicueta ambaye anahamia upande wa kulia huku Ivanovic akicheza kati. Anatarajia kupata wakati mgumu sana kutoka kwa Angel Di Maria ambaye anasikia kwa kasi nachenga za maudhi.


Angel di Maria (kulia) na Baba Rahman kwa naykati tofauti wakipasha misuli
0 comments:
Post a Comment