Tanzania Prisons imeendelea kufanya vizuri msimu huu baada ya kuwafunga mahasimu wao, Mbeya City kwa mabao 2-1 na kuwatupa nje ya Kombe la Shirikisho.
Prisons ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao mnamo dakika ya 39 kupitia kwa Mohammed Mkopi baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi maridhawa ya Sam Kimenya. Mbeya City walisawazisha kupitia kwa Joseph Mahundi.
Goli la pili la Prisons lilifungwa na mlinda mlango Benno Kakolanya katika dakika ya 82 baada ya kupiga mpira mrefu kutoka langoni na kutinga moja kwa moja wavuni na kumuacha kipa wa Mbeya City, Hannington Kasyebula ambaye alikuwa amesogea mbele ya lango lake, hivyo kushindwa kuokoa mpira huo.

0 comments:
Post a Comment