Monday, February 22, 2016

Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini ametetea uamuzi wake wa kujaza vijana kwenye mchezo wa jana wa kombe la FA dhidi ya Chelsea hali iliyopelekea kupokea kipigo cha mbwa mwizi cha magoli 5-1. Mchezo huo ulipigwa kunako dimba la Stamford Bridge.
Pellegrini alianzishwa wachezaji watano ambao walikuwa wakicheza kwa mara ya kwanza kabisa kwenye kikosi hicho akiwapumzisha nyota wake kwa ajili ya mchezo wa klabu bingwa dhidi ya Dynamo Kiev na mchezo wa Capital One dhidi ya Liverpool Jumapili.
Pellegrini amesema maamuzi yake ya kufanya hivyo yametokana na ratiba ngumu aliyonayo kwenye michuano mbalimbali inayoikabili timu hiyo.
'Moja ya vitu muhimu zaidi ni kusaidia timu za Uingereza ambazo zinacheza Ligi ya Mabingwa,' alisema.
'Siwezi kufanya 'risk' ya kutowafanya wachezaji wangu kuwa fiti kwa ajili ya safari ya leo ama kuzidi kuongeza majeruhi kwenye kikosi changu. Nadhani tumefanya suala sahihi kabisa. Haya ni maamuzi bora kwa kwa faida ya klabu.' aliongeza.

Ratiba ya michezo ya kombe la FA raundi ya 6 

Reading v Crystal Palace
Everton v Chelsea
Arsenal/Hull v Watford
Shrewsbury/Man Utd v West Ham
*Michezo hii itapigwa wikiendi ya March 11-14

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video