1. Utabiri wa vikosi vitakavyokuwa.

2.Sababu zinazowapa kiburi mashabiki wa Arsenal
- Arsenal ni moja ya vilabu viwili vilivyoifunga Leicester msimu huu.
- Arsenal wamepoteza mchezo mmoja tu kati ya tisa waliyokutana katika michuano yote.
- Leicester wameshindwa kabisa kuwafunga Arsenal kwenye michezo nane iliyopita na wameshinda mmoja tu kati ya ishirini waliyowahi kukutana.
3. Sababu zinazowapa kiburi Leicester
- Huu ni mwezi Februar na mpaka sasa wao ndiyo vinara wa ligi
- Wana wachezaji wawili ambao ni hatari mno na ndiyo wanaoamua mara nyingi matokeo ya timu hiyo (Jamie Vardy na Riyad Mahrez).
- 'The Foxes' wameshinda michezo yao mitatu ya nyuma ikiwemo dhidi ya Man City wikiendi iliyopita.
4.Mara ya mwisho kukutana
Septemba 26, 2015: Leicester 2-5 Arsenal (EPL)

FebruarI 10, 2015: Arsenal 2-1 Leicester (EPL)
Agosti 31, 2014: Leicester 1-1 Arsenal (EPL)
Mei 15, 2004: Arsenal 2-1 Leicester (EPL)
Desemba 6, 2003: Leicester 1-1 Arsenal (EPL)
5. Ubora wao kwa sasa
Arsenal - michezo 5 ya mwisho
Bournemouth 0-2 Arsenal (EPL)
Arsenal 0-0 Southampton (EPL)
Arsenal 2-1 Burnley (FA Cup)
Arsenal 0-1 Chelsea (EPL)
Stoke 0-0 Arsenal (EPL)
Leicester - michezo 5 ya mwisho

Manchester City 1-3 Leicester (EPL)
Leicester 2-0 Liverpool (EPL)
Leicester 3-0 Stoke (EPL)
Leicester 0-2 Tottenham (FA Cup)
Aston Villa 1-1 Leicester (EPL)
6. Mchezaji muhimu wa Arsenal

Alexis Sanchez
Katika magoli 5-2 waliyoshinda Arsenal raundi ya kwanza, Sanchez alifunga magoli matatu (hat-trick)
7.Mchezaji muhimu kwa Leicester

Kasper Schmeichel
Licha ya Mahrez na Vardy kuwa mwiba mchungu kwa timu pinzani msimu huu, Leicester inategemea ubora wa hali ya juu wa mlinda mlango wao Kasper Schmeichel ili kudhibiti mashambulizi ya Arsenal huku Vardy na Mahrez wakifanya kama ilivyozoeleka kwa upande wa timu pinzani.
8. Makocha wanasemaje?

Arsene Wenger juu ya wachezaji majeruhi: “Cazorla na Wilshere, siwezi kuwahesabu kama wapo katika wiki hii, labda kuanzia wiki tatu mpaka nne zijazo, lakini wengine wote wako kamili.
“Danny Welbeck anaendelea vizuri na kijiweka fiti zaidi ili aendani na kasi ya ligi kutokna na kukaa nje kwa muda mrefu, nadhani hana muda mrefu ataanza kucheza. .”

Claudio Ranieri
Leicester boss Claudio Ranieri juu ya umuhimu wa mchezo: “Pengine ni mchezo muhimu kwa Arsene Wenger, na sio kwetu. Presha kubwa ipo kwa timu nyingine. Arsenal wana presha kubwa kwa sababu Arsene Wenger hutumia pesa nyingi kila mwaka kununua wachezaji.
“Hatuna presha kwa sababu tumefanya kazi yetu. LengO letu limetimia - kinachokuja zaidi ya hapa ni kitu cha kujivunia. Watu wanataka kutupa presha kubwa kwa sababu mwanzoni walisema hawa kesho tu wataanza kupotea'.
“Lakini sasa wameanza kufikiri kuhusu sisi kuchukua ubingwa. Ni muhimu sana kuweka presha kwao kwa sababu wanatumia pesa nyingi sana na kama hawatachukua ubingwa, basi ni janga kwao.
“Kwa sasa hatuna presha tena, tulikuwa na presha mwanzoni wakati tuko juu lakini kadri siku zinavyosonga mbele wakati tukifanya vizuri, presha hatuna tena.
“Tupo karibu kutimiza ndoto zetu na mashabiki wetu na tunataka kuendelea kufanya vivyo hivyo, hakuna wa kutupa msukumo, tunajisukuma wenyewe.”
0 comments:
Post a Comment