Monday, February 22, 2016

Kinara wa mabao ligi kuu na fowadi tegemeo wa Simba, Mganda Hamisi Kiiza, juzi Jumamosi hakuwa kwenye ubora wake na hilo limethibitishwa na kocha wake, Jackson Mayanja ‘Mia Mia’ lakini akamkingia kifua kwa kile alichosema alikamiwa sana muda wote, ndiyo maana aliamua kumpumzisha.
Simba ililala kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga. Ikiwa imepoteza mechi yake ya kwanza baada ya kushinda sita mfululizo.
Kiiza hakufurukuta kabisa mbele ya Mtogo, Vincent Bossou ambapo alifanikiwa kupiga shuti moja tu mpaka anatolewa na nafasi yake inachukuliwa na Danny Lyanga.
Mayanja amesema Jumatatu: “Kweli hakuwa kwenye kiwango chake, hakufanya kile kilichotegemewa na wengi kwa wale wanaomjua Kiiza, lakini yote ni kutokana na alivyokamiwa na kukabwa na watu wawili muda wote.
"Yule Bossou alikuwa akimchezea kibabe, anapigwa, anaangushwa lakini hakuna maamuzi yaliyofanyika, ndiyo maana nikaamua kumjaribu Lyanga ambaye kidogo alionyesha uhai japo alikosa goli la wazi.” 
Chanzo:Salehjembe

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video