Sunderland wamevunja mkataba na Adam Johnson baada ya winga huyo kukutwa na hatia na mahakama kwa kosa la kujihusisha na masuala ya kimapenzi na mtoto.
Johnson (28) alikuwa akishutumiwa kujihusisha na masuala ya kimapenzi na mtoto mnamo Desemba 2014 na Februari mwaka jana. Lakini hata hivyo johnson, amekubali shtaka moja na kukaa mawili ya kufanya maepnzi na msichana wa umri chini ya miaka 16.
Taarifa kutoka kwa klabu inasomeka hivi: "Kutokana na Adam Johnson kukutwa na hatia, kuanzia leo klabu imesitisha mkataba wake mara moja."
Hata hivyo inasemekana na Adidas pia wamesitisha mkataba wa udhamini na winga huyo.
0 comments:
Post a Comment