Friday, February 19, 2016

UNAMKUMBUKA mtu mmoja anaitwa, Athuman Machuppa?Huyu jamaa Simba wanamfurahia sana, lakini Yanga hawapendi hata kumsikia kwa vile hajawahi kuwafanyia kitu kizuri zaidi ya kuwadhalilisha kwenye mechi za watani wa jadi ndani ya Uwanja wa Taifa.
Asipofunga yeye anatoa pasi ya kukuumiza. Ni miongoni mwa wachezaji wachache wenye heshima kubwa ndani ya Simba. Septemba 18, 2004 aliwauwa Yanga hapo Taifa, aliwapiga bao la usiku kabisa Simba ikashinda bao 1-0.
Aprili 17, 2005 alifunga tena bao la ushindi pale Morogoro, Simba ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-1. Sasa Machupa ameusoma mchezo wa Simba na Yanga wa kesho Jumamosi akawajaza sumu wachezaji wa Simba kwamba wanaweza kumpiga Yanga kweupe kabisa wala wasiwe na presha ila akatoa angalizo la watu wa kuwa nao makini.
Machuppa amewaambia wachezajii wa Msimbazi kuwa makini sana na wala wasivimbe vichwa. Amewatajia wachezaji watatu wa Yanga; Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima na Simon Msuva.
Machuppa ametoa tahadhari hiyo wakati Simba inaelekea kwenye mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga itakayochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam hiyo kesho.
“Utakuwa ni mchezo mgumu kwani Yanga inataka kumfunga Simba kwa mara ya pili msimu huu wakati Simba wanataka kulipiza kisasi cha mzunguko wa kwanza, kikubwa ni kwamba nidhamu ya mchezo ndiyo itakayozisaidia timu zote, mabeki na viungo wanatakiwa kuzingatia nidhamu kwa muda wote wa mchezo,” anasema Machuppa ambaye kwenye miezi ya hivi karibuni amekuwa akipiga dili zake Ulaya na Bongo.
“Yanga kwa upande wake inabebwa na wachezaji wazoefu lakini Simba ina chipukizi wengi ambao ndiyo wanajenga maisha, nawapa Simba nafasi kubwa zaidi ya kushinda kutokana na mwenendo wao wa hivi karibuni.”
“Hata Simba wana washambuliaji wazuri ambao wanaweza kufanya kitu, kuna Kiiza (Hamisi), Ajibu (Ibrahim) na Ndemla (Said) ila wanatakiwa kuwa makini na wachezaji hao watatu wa Yanga ni wajanja wajanja sana na muda wowote wanaweza kubadilisha matokeo,” alisema Machuppa
Mzunguko wa kwanza Yanga iliifunga Simba mabao 2-0 ambapo sasa wamejipanga kulipa kisasi huku kocha wa Simba, Jackson Mayanja, akiwa na imani kubwa ya kupata ushindi mnono kwa kile alichokieleza kuwa wachezaji wake wako fiti na morali ya hali ya juu na wanacheza soka safi.
Chanzo:Mwanaspoti


0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video