Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Ulinzi Stars ya Kenya Kevin'Jaobu"Ouma katika harakati zake enzi za uhai wake.
Tasnia ya mchezo wa soka nchini Kenya imegubikwa na simanzi baada ya kupata taarifa ya kusikitika ya kifo cha beki wa zamani wa timu ya ulinzi Stars, Kevin Ouma aliyefariki kwenye shambulizi nchini Somalia.
Beki huyo ambae alikuwa amestaafu soka baada ya kusumbuliwa na majeraha kwa misimu miwili na akachaguliwa na jeshi la Kenya kwenda kuimarisha Ulinzi nchini Somalia katika operesheni yake ya kulinda amani nchini Somalia ambapo jeshi hilo linashirikiana na vikosi vya AMISOM.
Tarehe Januari 15, mwaka huu, kundi la jeshi la Kenya lilikuwa katika mji wa El Ade, nchini Somalia lilishambuliwa na waasi wa Al Shabaab, tukio ambalo lilisababisha vifo la wanajeshi wa Kenya ikiwemo kifo cha Ouma.
0 comments:
Post a Comment