Saturday, February 20, 2016

Mayanja
Kocha Mganda wa Simba, Jackson Mayanja amekiri kuwa kweli aliwahi kumpigia simu mshambuliaji hatari wa Yanga, Amissi Tambwe.
Mayanja amesema alifanya hivyo wakati akiifundisha Kagera Sugar msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.
Mayanja amesema, lengo la kumpigia simu Tambwe kumshawishi ajiunge na Kagera Sugar ili iweze kung’ara katika ligi wakati huo.
“Ilikuwa wakati ule ambapo Simba ilimuacha Tambwe, nilimpigia simu nikitaka aje Kagera lakini Yanga wakaniwahi na wakamsajili na hadi leo unamuona anacheza kwao lakini ilibidi aende Kagera,” alisema Mayanja.
Akimzungumzia kuelekea mchezo wa leo wa Yanga na Simba, Mayanja alisema: “Kwa mechi kama hii, ni vigumu kusema nani atakuwa mtu hatari, unaweza kusema ni fulani lakini siku hiyo mtu mwingine ambaye hukumuwazia kabisa akawaathiri.
“Muhimu ni kujiandaa na kuamini kuwa Tambwe ni mtu hatari unapopambana naye uwanjani, tumejiandaa kwa yote hayo.”
Kabla ya kutua Simba, Mayanja amewahi kuzinoa Bunamwanya ya Uganda, Kagera Sugar na Coastal Union ya Tanga.
Chanzo:Salehjembe

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video