Tuesday, February 23, 2016

Wakiwa wamekutana na Barcelona kwa nyakati tofauti tofauti, Wenger amesema amejifunza namna ya kucheza na timu aina ya Barcelona.
'Kiukweli, bila shaka ugumu wa mchezo huu ni tofauti sana lakini ni vigumu zaidi kujiandaa dhidi ya Hull kuliko Barcelona, kwa sababu dhidi ya Barcelona kila mtu anajua uzito wa mchezo. 
Kinachotakiwa zaidi ni kutengeneza hali ya kujiamini kwa wachezaji, kwa sababu Barcelona wanapewa nafasi kubwa katika mchezo huu. 
Dhidi ya Hull unakuwa unahangaika kuwashawishi wachezaji kuamini ni mchezo muhimu na mgumu pia. 
Lakini kwa mchezo wa leo kila mtu anafahamu fika kwamba sote kwa pamoja tunatakiwa kuwajibika na kushirikiana kama timu, na hicho ndicho ninachijitahidi kufanya kwa sasa. imani na kujiamini ndio jambo la msingi'.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Arsene Wenger kucheza na Barcelona iliyo chini ya Luis Enrique. 
Mara nyingi alikutana na Barcelona iliyokuwa chini ya Pep Guardiola
'Kimsingi kwa sasa wana safu kali sana ya ushambuliaji. Hawamiliki sana mpira kama ilivyokuwa enzi za Guardiola kwa sababu walikuwa na Xavi kwenye eneo la kiungo  ambaye kwa mchezo mmoja alikuwa na uwezo wa kupiga pasi zaidi ya 100 na kuwafanya wamiliki mchezo kwa kiasi kikubwa. 
Kwa sasa nadhani wana timu ambayo wakati wowote wanaweza kufunga, hata kama hawajamiliki mpira sana lakini bado ni wakali. 
Na hii ilionekana dhahiri shahiri kwenye mchezo wa fainali ya UEFA mwaka jana dhidi ya Juventus - wakati matokeo yakiwa 1-1, walikuwa wakipata shida kidogo, lakini walipopata nafasi tu papo hapo wakafapata bao la pili. Hiyo ndiyo hatari yao kubwa. 
Hawamiliki sana mpira kwa sasa.
'Nilimjua Enrique kama mchezaji, kwa sababu alicheza dhidi yetu kwenye uwanja wa Wembley na alitufunga, nadhani nilikuwa bado kijana mdogo sana kwenye Ligi ya Mabingwa nikiwa kama kocha'.

TIMU ZILIZOING'OA ARSENAL HATUA YA 16 BORA KATIKA MISIMU MITANO MFULULIZO

2014-15 - Lost 3-3 (away goals) to Monaco
2013-14 - Lost 3-1 to Bayern
2012-13 - Lost 3-3 (away goals) to Bayern
2011-12 - Lost 4-3 to Milan
2010-11 - Lost 4-3 to Barcelona



0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video