Friday, February 26, 2016

Kocha wa JKT Mlale ya Ligi Daraja la Kwanza, Edgar Juvenary, ameweka wazi kutoridhishwa na uamuzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuipa nafasi Yanga ya kucheza michezo yake mingi ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Taifa kwa kuwa inakuwa na nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi.
Mlale ambayo inamilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa, ilifungwa mabao 2-1 na Yanga uwanjani hapo, juzi Jumatano ambapo kabla ya hapo Yanga iliichapa Friends Rangers katika uwanja huohuo mabao 3-0.
“Tumekubaliana na matokeo ya mchezo, tutajipanga zaidi kwa ajili ya msimu ujao lakini ningependa TFF iwe inaipeleka Yanga mikoani, mfano nao waje kule Songea wakutane na changamoto.
“Ikiwa kila siku hapa Taifa siyo sahihi kwa maana hatukupata nafasi hata ya kuufanyia mazoezi huu uwanja,” Juvenary alisema wakati akihojiwa na Salehjembe.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video