Friday, February 19, 2016

Licha ya Kocha wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm kujaribu kumshawishi nahodha wake na beki tegemeo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kufanya mazoezi, mchakato huo umeonekana kuwa mgumu na kuna uwezekano Cannavaro akakosa mechi ya kesho Jumamosi dhidi ya Simba.
Cannavaro aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu, alirejea uwanjani hivi karibuni lakini hajacheza mechi hata moja, alifanya mazoezi na wenzake kwa siku kadhaa lakini juzi hali ilibadilika na kushindwa kujumuika na wenzake katika mazoezi kwenye Uwanja wa Gombani.
Mara baada ya kufika uwanjani hapo, Cannavaro alijiunga katika dua ya pamoja lakini wakati mazoezi yakianza, akarejea katika benchi na kukaa, Pluijm akazungumza naye kwa dakika kadhaa lakini haikuwezekana kuinuka na kucheza. Hali hiyo iliendelea mpaka mwisho wa mazoezi. 
Pamoja na hivyo, hakuna kiongozi wala mtu yeyote wa benchi la ufundi aliyekuwa tayari kuzungumzia afya ya mchezaji huyo.
Yanga imekuwepo Pemba kwa kambi ya wiki moja ikijiandaa kuivaa Simba katika Ligi Kuu Bara, kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Chanzo:Championi

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video