Kocha wa Barcelona Luis Enrique amedai kuwa Lionel Messi na wenzake wako tayari kufanya maajabu yao kuelekea mchezo wa UEFA hatua ya 16 bora dhidi ya Arsenal utakaopigwa kwenye dimba la Emirates leo usiku.
Enrique amesisitiza kwamba uwepo wa safu yake kali ya ushambuliaji inayoundwa na Messi, Luis Suarez na Neymar - ambao mpaka sasa wameshafunga mabao 91 msimu huu- utarahisisha zoezi katika mchezo wa leo. 'Nisema nini kuhusu Messi, Suarez na Neymar? labda utakuwa ni upuuzi tu! ama cheche za maajabu. Hivyo ndivyo ninavyoweza kusema,' alisema Enrique.
Luis Enrique
Luis Suarez, Lionel Messi, Neymar
'Kiukweli mara zote nimekuwa nikifanya kazi kwa juhudi sana na vilevile nimekuwa nikipambana sana kuwa na safu bora ya ushambuliaji kwenye kikosi changu.
'Nimewashuhudia Arsenal kabla ya msimu huu. wakuwa wakicheza kwa kasi kwa muda fulani kutokana na aina ya wachezaji walionao.
'Lakini naamini tutajitahidi kuweka falsafa yetu ya kumiliki mpira hasa kwenye lango lao ili tuwezea kutimiza azma yetu.'
0 comments:
Post a Comment