Wednesday, February 24, 2016

Kocha wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm amesema kabla ya kuivaa Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara wikiendi iliyopita, alitenga muda wake kuwachunguza wapinzani wake hao hasa kwenye mbinu anazotumia kocha wao, Mganda, Jackson Mayanja.
Pluijm alisema baada ya kubaini Mayanja amekuwa na tabia ya kuanzisha viungo wengi naye akalazimika kubadili mfumo wake na kumtumia Pato Ngonyani katika kiungo cha timu hiyo kwa ajili ya kutibua mipango ya wapinzani wake na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Pluijm alisema baada ya kuangalia mechi kadhaa za Simba ndipo alipobaini mbinu za Mayanja kuwa amekuwa na tabia ya kujaza viungo wengi kati hivyo ikamlazimu naye abadili mfumo wake na kuiga mbinu hiyo kwa kuchezesha viungo wengi.
“Unajua niliwaangalia Simba jinsi wanavyocheza katika michezo yao ya nyuma ambapo nilibaini kuwa wanatumia mfumo wa kujaza viungo wengi kati hata ukiangalia kwenye mechi yetu walifanya hivyo.
“Baada ya kubaini hilo ndipo nikaona kuna haja kubwa ya kuweza kubadili aina ya uchezaji wetu kwa kumuongeza kiungo mmoja kati ambapo uliona Pato alianza kwenye mchezo ule.
“Na utaona namna gani kubadili mfumo kulivyoweza kuwadhibiti wapinzani ambao walishindwa kutengeneza mipira ya hatari langoni kwetu kutokana na kuweza kulikamata eneo lao hatari,” alisema Pluijm.
Katika mchezo huo Pluijm aliwatumia Pato, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke na Thabani Kamusoko katika eneo lao la kiungo.   
Credit:Salehjembe

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video