Kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas amesema walikuwa na presha kubwa katika mchezo wa jana wa FA raundi ya tano dhidi ya Manchester City kutokana kikosi walichopanga kujaa vijana wengi.
Kikosi cha City kilikuwa na vijana sita huku watano wakicheza kwa mara ya kwanza kwenye timu hiyo. Hali hiyo imetokana na kocha Manuel Pellegrini kuamua kupumzisha mastaa wake kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Dynamo Kiev lakini vile vile mchezo wa fainali ya Capital One Cup dhidi ya Liverpool.
"Lazima nikiri juu ya hili, ndiyo, ulikuwa ni mshtuko mkubwa kwetu", alisema. "Sijui kama huu ni mtazamo chanya ama sio… kwetu sisi pengine ulikuwa mtazamo hasi kwa sababu ilitufanya tuwe na presha zaidi.
"Endapo inatokea unafungwa na aina ya kikosi kama kile, kila mtu atawabeza".
0 comments:
Post a Comment