Kocha wa Manchester United Louis van Gaal anaamini kwamba, David de Gea atakuwa fiti katika mchezo dhidi ya Arsenal kesho.
De Gea amekosa michezo mitatu kutokana na majeraha ya goti yanayomkabili ambayo alipata wakati akipasha misuli kuelekea mchezo wa kombe la EUROPA dhidi ya Midtjylland Februari 18.
"Nataraji kumuona De Gea akirudi kwenye mchezo dhidi ya Arsenal kutokana na hali niliyomwona nayo Alhamisi," Van Gaal alisema.
"Smalling bado sijajua, lakini huwezi jua. Kuhusu Martial pia sina uhakika kwa sababu alipata majeraha yake kabla ya mchezo.
"Nimeongea na daktari wa timu na tayari anafuatilia kwa karibu maendeleo yake. Lakini hana majeha makubwa kama ambavyo wengi wanadhani."
0 comments:
Post a Comment