
David Luiz amewata Chelsea kuonesha heshima kwa Terry, akisisitiza kuwa suala hilo liko wazi kwa kila mtu kwamba mlinzi huyo anastahili mkataba mpya.
Beki huyo wa kati ambaye ni 'icon' wa Chelsea anatarajiwa kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu baada ya uongozi kumhakikishia kuwa hawatampa mkataba mpya.
"John pengine ndiyo mchezaji mkubwa wa muda wote wa Chelsea, klabu ni lazima imuoneshe heshima kubwa," alisema.
"Mwenyewe anasema kuwa anataka kubaki klabuni hapo, lakini klabu haijampa jibu lolote.
"Hivi sivyo ambavy unamfanyia mchezaji ambaye amejitolea kwa moyo wake wote katika kipindi chote alichokaa klabuni hapo. Mashabiki wanampenda John -Kama suala hili halitachukuliwa kwa umakini mkubwa basi, mashabiki hawatakuwa na furaha.
0 comments:
Post a Comment