
Thibaut Courtois amewaonya wachezaji wenzake wa Chelsea kumchunga sana mshambulizi wa Paris Saint-Germain Zlatan Ibrahimovic ili asilete madhara, kutokana na kuhofia kulipiza kisasi baada ya kupewa kadi nyekundu msimu wakati wa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa.
Ibrahimovic alitolewa nje kwenye mchezo wa marudiano wa hatua ya16 bora baada ya kumchezea rafu mbaya Oscar.
Hata hivyo licha ya kucheza pungufu kwa dakika nyingi, bado PSG walifanikiwa kuvuka hatua hiyo na kuingia robo fainali baada ya kuwa na wastani wa goli 3-3, hivyo kunufaika na goli la ugenini.
"Kwa kupewa kadi nyekundu katika mchezo dhidi yetu mwaka jana, Ibrahimovic atataka kulipiza kisasi dhidi ya wachezaji wa Chelsea," Courtois alisema
"Lakini kuna lingine, Chelsea nao watataka kulipiza kisasi baada ya kutolewa msimu uliopita.
"Mwaka hu tunataka kushinda mchezo huu. Kila klabu haipendi kutolewa katika raundi hii.
"Sisi sote tunataka kuendelea mbele zaidi katika michuano hii. Tunajua fika kwamba Paris wana timu imara sana, hivyo halitakuwa suala jepesi."
0 comments:
Post a Comment