Wednesday, February 24, 2016

Petr Cech amekiri kwamba wamehuzunishwa sana na matokeo mabovu ya mchezo wa jana dhidi ya Barcelona baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-0 katika kinyang'anyiro cha UEFA hatua ya 16 bora, mchezo wa kwanza uliopigwa kunako dimba la Emirates jijini London.
Magoli yote ya Barcelona yalifungwa na Lionel Messi.
Licha wageni Barcelona kumiliki mpira wa kiasi kikubwa kabisa , Arsenal walijikuta wakipoteza nafasi za wazi kupitia kwa Alex Oxlade-Chamberlain na Olivier Giroud. 
Cech , ambaye alifanya 'saves' za maana anasema kwamba walitakiwa kuwa na uchu wa magoli pindi washambuliaji wao walipokuwa wakifika langoni mwa Barcelona.

"Kama unacheza na moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kuwa mabingwa wa UEFA, unatakiwa kuzitumia kwa umakini wa hali ya juu nafasi zote unazopata", alisema.
"Nilidhani tlifanya vizuri sana mpaka tulipokuwa tumefungwa goli la kwanza. Tulikuwa tuna nafasi nzuri sana za kufunga , na nadhani hiyo ingeleta tofauti kubwa sana.
"Kitu kikubwa ambacho hatukufanikiwa ni kuzitumia kwa usahihi nafasi tulizopata. Katika mchezo kama huu unahitaji kuwa mwepesi sana kuliona lango la wapinzani wako.
"Walipata nafasi tatu ama nne kama ambavyo sisi pia tulipata, lakini tofauti ni kwamba wao waliweza kufunga lakini sisi hatukufanya hivyo".

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video