Friday, February 12, 2016

Nahodha wa zamani wa Italy Fabio Cannavaro amefukuzwa ukocha kunako klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia.
Cannavaro alipewa michezo 22 ili kuisaidia Al-Nassr kutetea taji lake katika ligi ya nchi hiyo almaarufu Saudi Pro League, lakini kibarua chake kimeota mbawa baada ya michezo 12, hasa baada ya kipigo cha mabao 4-3 kutoka kwa Najran ambao wako nafasi ya tatu kutoka mkiani hapo jana.
Cannavaro ambaye hapo awali alikuwa akiwanoa mabingwa wa China Guangzhou Evergrande na kuachana nao mwezi June, na kuchukua mikoba ya Jorge da Silvan mwezi Oktoba mwaka jana kunako vigogo hao wa ligi ya Saudi Arabia, ameshindwa kabisa kuonesha umahiri wake na kuishia kutimuliwa.
Al-Nassr wapo nafasi ya sita, wakiwa na pointi 18 nyuma ya vinara Al Hilal, huku wakiwa wameshinda mara moja tangu kuingia kwa mwaka 2016 baada ya kutawazwa mabingwa mwezi Mei mwaka jana.
Mkataba wa Cannavaro na na klabu ya  Al-Nassr ulitakiwa kuisha mwishoni mwa msimu huu

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video