Kuna tukio la aina yake limetokea kwenye mchezo wa soka kwenye ligi ya Ireland Kaskazini siku ya Jumamosi (jana) wakati wa pambano kati ya Linfield dhidi ya Glenavon.
Mchezo ho ulimalizika kwa penati tatu kupigwa ndani ya dakika 90 za mchezo. Kila upande ulipata bao kwa njia ya mkwaju wa penati.
Aaron Burns aliifungia Linfield bao la kuongoza kipindi cha kwanza, Andy McGrory akasawazisha dakika ya 80 kipindi cha pili.
Wakati mchezo huo ukielekea ukingoni, golikipa wa Linfield Ross Glendinning alimwangusha striker wa Glenavon ndani ya box kitendo kilichopelekewa kutolewa kwa kadi nyekundu na mwamuzi wa mchezo huo.
Mbali na golikipa huyo kuoneshwa kadi nyekundu, Linfield walikuwa wameshamaliza nafasi zao za wachezaji wa akiba (subs). Kilichofanyika ni beki wa kati wa timu hiyo Mark Haughey kuvaa glove na kusimama langoni kwa dadkika zilizosalia.
Haughey alifanikiwa kucheza mkwaju wa penati uliopigwa na Kevin Braniff na kuinusuru timu yake kupokea kichapo cha dakika za majeruhi.
Video
0 comments:
Post a Comment