Mchezaji kiraka wa Simba, Abdi Banda hatakuwepo katika kikosi cha timu hiyo kitakachovaana na Yanga Jumamosi ya Wikiendi hii uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Banda ambaye anamudu nafasi zote za kiungo na beki aliposti picha katika ukurasa wake wa facebook akieleza kuwa atakuwa nje kwa kipindi kisichopingua miezi miwili kutokana na majeraha ya goti.
Banda aliandika ujumbe uliosomeka hivi: “Dah nitamis sana kurudi uwanjani, miezi miwili ni mingi sana, dah ila ntapona.”
Ujumbe wa beki huyo, uliendana na picha yake aliyoiweka akiwa amelala kitandani hospitalini akifanyiwa vipimo.
Lakini cha kushangaza baada ya muda fulani picha hiyo haikuonekana tena, kwa maana ya kwamba aliifuta posti hiyo.
0 comments:
Post a Comment