
Joleon Lescott alitweet picha ya gari yake aina ya Mercedes yenye thamnai ya paundi 121,000 baada Aston Villa kupokea kpigo cha magoli 6-0 kutoka kwa Liverpool

"Huu ndiyo ufafanuzi alioutoa Lescott juu ya Tweet hiyo na kusema kuwa picha ya gari hilo alitweet bahati mbaya.
Lescott anasema: Mimi sio moja ya wanaopenda kutweet baada ya mchezo ama iwe tumepata matokeo mabaya au mazuri lakini mimi na wenzangu kwa ujumla tungependa kuomba radhi kwa matokeo mabovu. Liverpool ni wako na walikuwa vizuri zaidi yetu leo, lakini haimaanishi kuwa tunaepuka lawama kutokana kutojituma ipasavyo kwa dakika 90. Kwa mara nyingine tena tunaomba radhi kwa mashabiki wote."
"Ningependa kuongeza kitu juu ya tweet ya iliyoonekana kwenye akaunti yangu ambayo ilihusisha picha ya gari, niseme tu kwamba ilikuwa ni bahati mbaya, ilitokea nikiwa kwenye gari wakati simu yangu ikiwa mfukoni."

Joleon Lescott akisikitika baada ya Aston Villa kifungwa na Liverpool magoli 6-0 jana katika uwanja wa Villa Park.
0 comments:
Post a Comment