Friday, February 26, 2016

Kocha Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja, ameandaa mikakati kabambe kwa kubadili gia kwa kuhakikisha anafanya mabadiliko katika kikosi chake ili kirejee kwenye makali yake baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Yanga.
Simba ilipoteza mchezo huo na hivyo kushuka kutoka nafasi ya kwanza hadi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, ikiwa nyuma ya Yanga na Azam hali ambayo inatoa hofu kwa Wanamsimbazi kuelekea katika mbio za ubingwa.
Mayanja amesema kuwa anahitaji kufanya tathmini ya kikosi chake kwa ajili ya kufanya mabadiliko ili kuja na kasi nyingine kwa kukipanga upya ili kuweza kufanya vizuri katika michezo inayofuata ili kujiweka katika nafasi nzuri ya msimamo wa ligi na ikiwezekana kutwaa ubingwa.
“Nitakaa chini na kikosi changu kuona ni jinsi gani naweza kufanya mabadiliko kwa kufanyia kazi yale ambayo yamejitokeza katika mchezo huo ili kukifanya kuwa bora na kushinda katika mechi zinazofuata.
“Nahitaji kukaa chini na kujadili kuona wachezaji wangapi wana kadi ambao watakosa mchezo unaofuata na wachezaji majeruhi kisha niweze kukipanga kikosi changu kwa ajili ya maandalizi katika mechi zinazofuata kwani bado tunayo nafasi ya kuwania ubingwa na lolote linaweza kutokea,” alisema Mayanja.
Credit:Salehjembe

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video