Louis van Gaal amekiri kwamba mashabiki wa Manchester United walikuwa sahihi kuwatolea lugha chafu baada ya kupokea kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa FC Midtjylland ya Denmark kwenye michuano ya EUROPA Denmark
Mashabiki wa United walikuwa wakiimba 'f*****g s**t' kwa kurudia rudia hasa baada ya pambano lao kumalizika .

Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal akishangaa baada ta timu yake kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Midtjylland.

Wachezaji wa Man United wakiwa na fedheha baada ya kipigo.
Mashabiki wana haki ya kutukosoa. Ni lazima tuboreshe mchezo wetu ili mashabiki warudi tena kutupa sapoti.
'Wanafedheheka kama ilivyo kwa upande wangu pia. Nawashukuru sana mashabiki waliotusapoti lakini tulikuwa tukitaka ushindi na tunapaswa kufanya hivyo katika uwanja wetu wa Old Trafford ili kufuzu kwa hatua inayofuata. Tunapaswa kufanya hivyo japo si rahisi.'
0 comments:
Post a Comment