Tuesday, February 23, 2016

Arsenal v Barcelona: Champions League match preview & predicted line ups
Timu mbili zinazocheza mpira wa kuvutia duniani zinakutana katika dimba la Emirates usiku wa leo, si nyingine bali ni Arsenal ambao ndiyo wenyeji wa mchezo huo dhidi ya Wakatalunya Barcelona, pambano hilo ni la hatua ya 16 bora.
Wakiwa na utatu mtakatifu katika safu yao ya ushambuliaji inayoundwa na Messi, Suarez na Neymar, Baarcelona ndiyo wanapewa nafasi kubwa sana si tu ya kufuzu bali kuibuka na ushindi katika michezo yote miwili.
Lakini, si jambo rahisi kuiondoa Arsenal katika kinyang'anyiro hiki kwani pia wana kikosi chenye wachezaji wenye viwango vya kutisha kama Mesut Ozil, Alexis Sanchez na wengineo, hivyo ubora wa kikosi chao ni tishio pia kwa Barcelona.
Ushindi usioridhisha dhidi ya Las Palamas wakifuatiwa na mechi ngumu za Atletico na Real Madrid, inawafanya Barcelona kuwa na kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha wanachanga vyema karata zao ili kubaki katika kinyang'anyiro katika sehemu zote mbili (La Liga na UEFA), hivyo kuchagiza mechi ya leo kutokuwa rahisi hata kidogo.
Swali kubwa kwa kocha wa Barcelona Luis Enrique litakuwa, ni nani wa kuanza katika eneo la kiungo, je, Sergio Busquets, Sergi Roberto ambaye hapewi nafasi sana, Andres Iniesta ama Ivan Rakitic. Arda Turan hatakuwepo.
Golini anaweza kusimama Marc ter Stegen ambaye ndiyo amekuwa mlinda mlango wa Barca kwenye michuano hii, lakini kiwango bora cha Claudio Bravo ni wazi kuwa anaweza kusimama yeye langoni kwa siku ya leo.
Kwa upande wake Arsene Wenger tayari ameshazungumzia mchezo huo
Beki wa kati Gabriel hatakuwepo kutokana na kusumbuliwa na majeraha, hivyo Per Metersacker akisaidia na Laurent Koscielny watakuwa na jukumu kubwa la kumlinda kipa wao Petr Cech, huku wakisaidiwa na Nacho Monreal upande wa kushoto na Hector Bellerin kulia huku katika wakipata msaada mkubwa kutoka kwa kiungo kisiki Mfaransa Francis Coquelin
Ikumbukwe pia Leo Messi hajawahi kumfunga Petr Cech na hivyo kuwa na mchuano mkali kwa wawili hao kuonyesha umwamba.
Arsenal mbele inamtegemea Olivier Giroud, lakini vile vile kuna Danny Welbeck ambaye pia kama atapewa nafasi anaweza kufanya mambo makubwa zaidi kutokana na kasi yake na uwezo wa kumiliki mpira.
Mesut Ozil na Alexis Sanches ndiyo jicho la Arsenal kwa siku ya leo kutokana na kuwa na madhara makubwa kwa timu pinzani pindi wawapo kwenye ubora wao

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video