
Wakatti Arsenal wakijiandaa kuwakaribisha Leicester katika dimba la Emirates kesho, vijana hao walio chini Mfaransa Arsene Wenger wanaonekana kukabiliwa na matatizo makubwa sana.
Endapo watashinda mchezo wao wa Jumapili dhidi ya vinara Leicester, watakuwa wamepunguza wigo na kubaki na pengo la pointi mbili tu. Nafasi ambayo itaamsha ari yao katika mbio za kusaka ubingwa msimu huu.
Hata hivyo kama ilivyoonekana kwenye msimamo wa ligi, Arsenal wanaonekana kuwa na udhaifu mkubwa katika safu yao ya ushambuliaji.
Kimsingi, linapokuja suala la kuzitumia vizuri nafasi wanazopata ili kupachika mabao, Arsenal kwa sasa ndiyo timu dhaifu kuliko timu zote zilizopo Ligi nchini Uingereza.
Uwezo wa Arsenal katika kuzitumia kwa usahihi nafasi za wazi wanazopata msimu wa 2015/16

Kwa msaada wa Opta, mtandao huu umejaribu kuangalia ni namna gani timu zilizopo ligi kuu England waamekuwa wakizitumia kwa uzuri nafasi zao wanazopata hasa zile nafasi za karibu na goli (close range).
Arsenal imeonekana kuwa ni dhaifu sana katika hilo. Wana asilimia 32.1.
Angalia kwa umakini jedwali hili.
0 comments:
Post a Comment