Saturday, October 10, 2015

Mlinda lango wa Arsenal Petr Cech, amesema kuwa kocha wake Arsene Wenger na hasimu wake Jose Mourinho mara zote wamekuwa wakiingia katika migongano kutokana na na wote kuwa na hulka zinazofanana.
Wenger na Mourinho wamekuwa katika msuguano mkali pale wanapokutana, hasa ukizingatia kuwa katika michezo 15 waliyokutana, Wenger ameibuka mshindi mara moja tu ambao ni mchezo wa Ngao ya Jamii uliopigwa mnamo mwezi Agosti mwka huu.
Mourinho ameshawahi kumwita mpinzani wake kuwa ni 'bingwa ama mtaalamu wa kushindwa' na wawili hao pia wameshawahi kukunjana mashati wakati timu zao zilipokutana msimu uliopita katika dimba la Stamford Bridge.
Cech - ambaye alijiunga na Arsenal akitokea Chelsea mwezi Juni mwaka huu - alisema kuwa njaa ya ushindi kwa wawili ndio sababu kubwa ya kutokuwa na maelewano mazuri.
"Hili swali ni zuri zaidi ukiwauliza wenyewe. Lakini, ndio, waktai mwingine chanya mbili haziwezi kuleta chanya," alisema.
"Ufanano wao ni kwamba kila mmoja ana njaa ya ushindi. Kama ukimuuliza ask Jose Mourinho au Arsene Wenger kama wanataka kushinda kila kitu: kila mtu atakwambia ndio.
"Unaweza kuona kwamba kila mtu hapendi kupoteza mechi anazocheza na nadhani ndio kitu ambacho unahitaji kuwa nacho endapo unataka kufanikiwa.l."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video