Friday, October 2, 2015


Kocha wa Arsenal Arsene Wenger leo ametishia kusitisha mkutano na waandishi wa habari baada ya kukoselewa kwa maamuzi yake ya kumpanga David Ospina goli na kufungwa goli la kizembe katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Olympiacos uliopigwa Jumanne wiki hii ambao Arsenal walifungwa 3-2 nyumbani. 
Ospina alifanya kosa la kizembe baada ya kuutemea mpira ndani ya lango lake na kupelekea Wenger kukumbana na maswali ya kukera kutoka kwa waandishi, kwamba ni kwa sababu gani aliamua kumuanzisha Mkolombia huyo badala ya kipa namba 1 Petr Cech, katika mchezo huo wenye umuhimu mkubwa kwa mustabali wa kundi lao.
Hata hivyo, Mfaransa huyo amepinga vikali wote wanamkosoa kuhusu uteuzi wake wa kikosi, na kusisitiza kuwa "hakuna anayefanya uchambuzi wa kimahesabu".
"Sikiliza, achana na hizo habari, vinginevyo tuvunje mkutano huu," Wenger aliwaambia waandishi. "Nadhani kama waandishi mnakosa ubunifu, na kuishia kufuata mkumbo tu, kitu ambacho kinaunaudhi sana.
"Kama ukiuliza kuhusu Ospina, itabidi nitilie shaka ujuzi wako katika soka. Watu hawafanya uchambuzi makini. Nimesikia wachambuzi wakikosoa kitu kimoja tu, na kila mtu ameangukia hapo hapo.
"Kweli. Ndio, kipa alifanya makosa, lakini bado tungeweza kushinda ule mchezo."
Arsenal wanajiandaa na mchezo dhidi ya Manchester United Jumapili wikiendi hii, huku wakiwa na alama tatu pungufu ya vijana wa Louis van Gaal, na tayari Wenger ameshathibitisha kutokuwepo kwa mlinzi wake wa kati Laurent Koscielny siku ya mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Emirates.
"Laurent Koscielny atakuwan nje ya uwanja kwa kipindi kinakadiriwa kufikia takribani wiki tatu," aliongeza.
"Mathieu Flamini na Mikel Arteta pia watakuwa nje huku kiungo chipukizi na tegemezi kwa sasa Francis Coquelin anatarajiwa kuwa fiti."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video