Thursday, October 8, 2015


Straika wa Kenya, Michael Olunga akishangilia moja ya goli 
Tanzania na Kenya zimeanza kwa ushindi kampeni ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
Tanzania iliicharaza Malawi 2-0 katika mechi iliyochezewa jana uwanja wa Taifa,  jijini Dar es Salaam.
Bao la kwanza la Taifa Stars lilifungwa na Mbwana Samata dakika ya 18 na la pili likatiwa kambani na Thomas Ulimwengu dakika ya 22.
Nchini Mauritius, Kenya walikuwa na mteremko, wakiondoka na ushindi wa 5-2 dhidi ya wenyeji wao.
Harambee Stars ilitangulia kufunga kupitia Johanna Omolo dakika ya 18, Ajub Masika dakika ya 23 na Shakava dakika ya 49.
Mauritius hata hivyo walijikakamua na nusura wafanye mapinduzi baada ya kupata mabao mawili kupitia Sophie dakika ya 66 na Bru dakika ya 78.
Lakini Kenya walidhibiti tena mchezo kupitia bao la Michael Olunga dakika ya 87 na bao la pili la Omolo dakika ya 82.
Mechi kati ya Sudan Kusini na Mauritania, ambayo ilikuwa yao ya kwanza kabisa katika dimba la Kombe la Dunia, ilisimamishwa kutokana na mvua kubwa.
Wakati wa kusimamishwa kwa mechi hiyo mjini Juba, timu zote mbili zilikuwa sare 1-1, bao la Sudan Kusini likitoka kwa Dominic Abui Pretino na la Mauritania Boubacar Bagili.
Katika mechi nyingine, Burundi walilaza Ushelisheli kwa bao moja bila.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video