Wednesday, October 7, 2015

Thomas Ulimwengu (kulia) akimkimbilia Mbwana Samata kushangilia goli la pili baada ya kuifungia Stars wakati ikicheza dhidi ya Malawi

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ chini ya kocha mzalendo Charles Boniface Mkwasa leo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Malawi kwenye mchezo wa awali uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Mbwana Samata alianza kuiandikia Stars goli la kwanza dakika ya 19 kipindi cha kwanza akiunganisha pasi ya mchezaji mwenzake wa TP Mazembe Thomas Ulimwengu.
Stars baada ya kupata goli hilo waliamka na kuanza kucheza mpira na kutawala mchezo kwa asilimia nyingi katika kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini nafasi hizo hazikutumiwa ipasavyo kwani bado walipoteza nafasi nyingi za kufunga.
Mbwana Samata (aliyepiga goti) akishangilia kwa kufuta kiatu cha Thomas Ulimwengu baada ya kufunga goli la kwanza akipokea pasi toka kwa Ulimwengu

Thomas Ulimwengu aliiandikia Stars bao la pili dakika ya 22 kipindi cha kwanza akimalizia mpira uliomshinda kipa wa Malawi uliopigwa na Haji Mwinyi na kuihakikishia timu hiyo kupata ushindi wa kwanza tangu imeanza kunolewa na Mkwasa aliyepokea kijiti hicho toka kwa kocha Mart Nooij aliyetimuliwa mwezi Julai mwaka huu.
Kabla ya mchezo wa leo, Stars ikiwa chini ya kocha Mkwasa imetoka sare kwenye mechi mbili za mashindano na kupoteza mchezo mmoja wa kirafiki.
Mrisho Ngassa (kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa Malawi wakati wa mchezo kati ya Stars dhidi ya Malawi kuwania kukata tiketi ya kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2018
Sare ya kwanza ilikuwa ni dhidi ya Uganda mchezo uliochezwa Uganda kuwania kufuzu kucheza fainali za Afrika kwa wacheaji wa ligi za ndani (CHAN) huku wakitoka sare ya bila kufungana dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika.
Stars ikiwa chini ya Mkwasa ilipoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Libya kwa goli 2-1 wakati ikiwa Uturuki kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video