Friday, October 9, 2015

Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi. 
YANGA inasaka Kocha Msaidizi ambaye ni kiboko ya Simba  atakayekuwa mkali zaidi ya Boniface Mkwassa aliyepata ajira ya kuifundisha Taifa Stars.
Ni kwamba muda wowote kuanzia sasa, klabu hiyo itampa mkataba Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi, ambaye ni kiboko ya Wekundu wa Msimbazi.
Tangu Mbeya City ipande daraja kucheza Ligi Kuu Bara ikiwa chini ya Mwambusi, Simba haijawahi kupata ushindi wowote kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na hata ugenini Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Katika rekodi hizo za ligi, kwa Mbeya City huu ni msimu wao wa tatu kushiriki ligi ambapo msimu wao wa kwanza wakiwa Uwanja wa Taifa, ilitoka sare ya 2-2 na Simba huku ikilazimisha sare nyingine ya 1-1 katika mechi ya marudiano iliyochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
City ambao inajiandaa kuikaribisha Simba wiki ijayo kwenye mechi ya Ligi hiyo, msimu uliopita iliifunga Simba mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa na kupata ushindi mwingine wa 2-0 ikiwa nyumbani Mbeya na rekodi hiyo imeivutia Yanga na kuamua kumpa ulaji Jangwani.
Juzi Jumatano, Mwambusi alikuwa miongoni mwa makocha walioshuhudia mechi ya Taifa Stars na Malawi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia ambapo Stars iliibuka na ushindi wa bao 2-0, baada ya mechi hiyo Mwambusi alikutana na viongozi wa Yanga.
Habari za ndani kutoka Yanga, zinasema kuwa Mwambusi alifanya kikao na viongozi wa Yanga kutoka Kamati ya Mashindano, Kocha wao Hans Pluijm huku ikisemekana kuwa Katibu Mkuu, Jonas Tibahora alihudhuria kikao hicho kilichofanyika katika hoteli moja jijini Dar es Salaam na kumtambulisha Mwambusi kwa Pluijm.
“Kulikuwa na mapendekezo ya makocha watatu; Mbwana Makata, Felix Minziro na Mwambusi, kocha Pluijm alipendekeza msaidizi wake atoke Tanzania na awe anajua kuzungumza vizuri kiswahili ili kurahisisha maelewano kati yake na wachezaji,” kilisema chanzo chetu.
“Mbali na hilo alitaka kocha ambaye ni mzoefu wa ligi na amepata mafanikio makubwa huko anakotoka, hivyo Mwambusi ni miongoni mwa makocha ambao wana sifa hiyo, jana (juzi Jumatano) walikubaliana kila kitu na kinachosubiriwa sasa ni kusaini mkataba tu.”
Chanzo hicho kililiambia Mwanaspoti kuwa zoezi la kusaini mkataba huo na Mwambusi huenda likafanyika kabla ya mechi yao na Azam FC itakayochezwa Oktoba 17 ingawa Mwambusi tayari amesharejea Mbeya akikabiliwa na kibarua wiki ijayo dhidi ya Simba.
Habari zaidi zinasema kuwa Mwambusi ataisaidia Yanga kwa kiasi kikubwa kutokana na uzoefu wake na alivyoweza kuitengeneza Mbeya City ambapo pia ni mtaalamu zaidi wa utimamu mwa mwili wakati Pluijm yeye ni mtaalamu wa ufundi.
Lakini jambo jingine ambalo limeivutia Yanga kwa Mwambusi, ni nidhamu aliyonayo na umakini wa kazi yake ambao unaendana na Pluijm.


Endapo Mwambusi atasaini mkataba na Yanga, basi litakuwa pigo kwa Mbeya City ambapo Katibu Mkuu wa timu hiyo, Emmanuel Kimbe, amesema kuwa watalitolea ufafanuzi endapo watapewa taarifa za kuondoka kwa Mwambusi kimaandishi kwani bado wana amini ni kocha wao.

 “Tumesikia tu, ila bado hatuna uhakika kwani hatujapewa taarifa kimaandishi, hivyo hatuwezi kuzungumzia lolote,”alisema.
Credit:Mwanaspoti

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video