Saturday, October 10, 2015

KOCHA maarufu nchini, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, amesema kamwe hawezi kuhusishwa na mpango wa kuifundisha Yanga kutokana na imani potofu iliyojengeka miongoni mwa wapenzi wa klabu hiyo na hata wale wa Simba kutowaamini watu wa upande mwingine.
Yanga kwa sasa ipo katika mchakato wa kusaka kocha msaidizi wa kubeba mikoba ya Charles Boniface Mkwasa, aliyepewa mkataba wa kuinoa timu ya Taifa, Taifa Stars na Julio akiwa ni mmoja wa wenye sifa ya kuwa msaidizi wa Hans van der Pluijm.
Akizungumzia taarifa hizo jana, Julio alisema hata kama atatakiwa Yanga, kamwe hawezi kuifundisha timu hiyo mpaka kufa kwake kutokana na dhana hizo za mashabiki.
“Mimi ni kocha, kazi yangu kufundisha mpira, lakini kamwe siwezi kuifundisha Yanga hata itokee vipi,” alisisitiza Julio.
Alisema ni ngumu kwa mtu ambaye ameitumikia Yanga au Simba muda mrefu kuaminiwa na kupewa nafasi nyeti katika upande wa pili wa klabu hizo mbili kongwe hapa nchini.
Julio alisema akiwa ameichezea Simba kwa muda mrefu pamoja na kuifundisha, hawezi kuaminiwa kuinoa Yanga kama ilivyo kwa kocha mwenzake, Fred Felix Minziro aliyekuwa kipenzi cha Wanajangwani kupewa nafasi Msimbazi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video