Mkenya anayechezea soka ya kulipwa katika klabu ya Southampton nchini Uingereza, Victor Mugubi Wanyama ametupilia mbali harakati za uhamisho wake ambao haukufanikiwa alipotaka kuelekea kilabu ya Tottenham na sasa anasisitiza kuwa anaijali timu ya Southampton pekee.
Wanyama anayechezea safu ya kati alitaka kuhamia Tottenham ili kujiunga tena na mshauri wake Mauricio Pochettino katika klabu ya Spurs kwa kufanya mgomo mnamo mwezi Agosti.
Lakini mkufunzi wa klabu hiyo Ronald Koeman alisisitiza kuwa nyota wake si wa kuuza ili kuhakikisha kuwa anasalia St. Marys baada ya Wanyama kukataa kucheza dhidi ya Norwich.
Wakuu wa Southampton wana matumaini ya kumpatia kandarasi mpya mchezaji huyo kwa miaka mingine mitano.
Wanyama ameonekana akicheza vyema na kuiwezesha Southampton kupanda katika jedwali la ligi ya Uingereza.
0 comments:
Post a Comment