Jaji mmoja nchini Uhispania ameagiza kwamba nyota wa timu ya Barcelona na Argentina Lionel Messi, ni sharti ashtakiwe kwa mashtaka ya kuibia mamlaka ya ushuru zaidi ya dola milioni 4.
Iwapo atapatikana na hatia atakabiliwa na kifungo cha miezi 22.
Jaji huyo amesema kuwa Messi na baba yake Jorge, lazima wawasilishwe mahakamani kwa madai kwamba walificha malipo yaliyotokana na haki zake za mauzo huko Belize na Uruguay.
Jaji huyo pia alikataa ombi kutoka kwa kiongozi wa mashtaka kwamba Jorge pekee ambaye alisimamia masuala ya fedha ya mwanawe ndiye alipaswa kufunguliwa mashtaka.
Miaka miwili iliyopita wakati mashtaka hayo yalipofunguliwa, Messi na babake walilipa dola milioni tano kwa mamlaka ya ushuru.
0 comments:
Post a Comment