Kocha wa Taifa Stars , Boniface Mkwasa
SIKU chache tu tangu apewe kibarua cha muda mrefu cha kuinoa Taifa Stars, Kocha Boniface Mkwasa, ameikumbuka klabu yake ya zamani, Yanga, akisema kuwa hataisahau kwani ndiyo iliyompa mchongo mzima Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupata ajira hiyo.
“Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipoishukuru Yanga iliyonipa ushirikiano kwa muda nilikaa nao, wakati nakinoa kikosi chao nikiwa chini ya Mholanzi Hans Pluijm, huko ndiko TFF iliponikuta na kuona nastahili kupewa kazi hii kwa maendeleo ya taifa,” alisema.
Kocha Mkwasa aliitoa wasiwasi Yanga kuwa kama itakuwa inahitaji msaada wake yu tayari kuutoa, kwani ameondoka kwa amani baada ya kukabiliwa na majukumu ya kitaifa kwa sasa. “Nitumie muda huu kuomba radhi kwa mashabiki wa Yanga, viongozi na wachezaji kama kuna mapungufu nilifanya wanisamehe, kwa upande wangu hakuna walichonikosea,” alisema.
Alitoa wito kwa Watanzania kushirikiana naye kwa ajili ya kuleta maendeleo ya Stars kwani mchango wao unahitajika ili kuweza kufika mbali zaidi.
“Ushirikiano wa Watanzania ndiyo utakaoleta maendeleo na tunaweza kufika mbali kwani kila kitu kinaenda kwa hatua, naamini ipo siku tutafika mbali,” alisema.
Credit:Mwanaspoti
Credit:Mwanaspoti
0 comments:
Post a Comment