KLABU ya Yanga imeamua kuja kivingine msimu huu ikitaka kuzichanganya timu watakazokutana nazo kwa ‘style’ mbalimbali za uchezaji lakini zaidi ikiwa ni ufungaji mabao.
Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm, amekuwa akisifika kwa mtindo wake wa soka la kushambulia kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho.
Mfumo huo ndio hasa unaomwezesha Pluijm kupata ushindi mnono kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo alikuwa akishinda hadi mabao 8-0 kama alivyoifanya Coastal Union katika mchezo wa marudiano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa timu hiyo raia wa Zimbawe, Donald Ngoma, ndiye aliyevujisha mkakati wao huo akisema katika kuusapoti kwa vitendo, wataanza na mtindo wa kufunga mabao ya mapema zaidi kabla timu pinzani hazijajipanga vizuri ili kuzichanganya.
Akizungumza na BINGWA, Ngoma alisema kuelekea mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara Jumapili dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa, Ngoma aliyetua Yanga msimu huu akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, alisema moja ya mikakati yake ni kuweka rekodi kuwa mchezaji wa kwanza wa kigeni kufunga bao la mapema zaidi.
0 comments:
Post a Comment