Wednesday, September 16, 2015

Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, leo imeendelea tena ambapo, Mabingwa soka nchini Yanga wamefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Wajelajela Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya, mchezo uliopigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga ambao walionekana kutawala wakati wote wa mchezo, walikuwa na kila dalili za kuibuka na ushindi katika mchezo huo, ambapo walianza mpira kwa kasi na kukosa nafasi kadhaa za wazi kabisa mwanzoni mwa mchezo kupitia washambuliaji wake Amissi Tambwe na Donald Ngoma.
Yanga walifanya shambulizi la kwanza kupitia Msuva, mnamo dakika ya 25 lakini shuti lake lilipaa juu langoni mwa Prisons.
Juhudi za Yanga zilizaa matunda mnamo dakika ya 27, baada ya kiungo mkabaji Mbuyu Twitte kumalizia mpira uliopanguliwa na kipa wa prisons kutokana na faulo iliyopigwa kwa umaridadi wa hali ya juu na Haruna Niyonzima baada ya Deus Kaseke kufanyiwa madhambi.
Yanga walipata bao la pili kupitia kwa Amissi Tambwe kwa kichwa mnamo dakika ya 45 baada ya kumalizia mpira uliotemwa na kipa wa Prisons kutokana na mpira wa faulo nzuri iliyochongwa na kiungo raia wa Zimbabwe Thabani Scara Kamusoko.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Yanga walikuwa mbele kwa magoli 2-0.
Katika kipindi cha pili Yanga waliendeleza wimbi lao la mashambulizi kwa lango la Prisons na almanusra tu Amiss Tambwe afunge bao la tatu lakini mpira wa kichwa aliopiga dakika ya 58 ukapaa sentimeta chache tu kutoka lango la Prisons.
Yanga walipata bao tatu kwa mkwaju wa penati kupitia Kwa Donald Ngoma mnamo dakika 60 baada ya Msuva kukwatuliwa katika eneo la hatari na beki wa Prisons James Josephat na kuzawadiwa kadi nyekundu na papo hapo.
Tambwe alikosa tena bao dakika ya 74 baada ya shuti lake kuokolewa na kipa wa Prisons.
Mpaka mwisho wa mchezo Yanga waliondoka na ushindi huo mnono wa mabao 3-0 na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa Ligi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video