Arsene Wenger ametetea sera yake ya usajili, licha ya Arsenal kushindwa kununua mchezaji yeyote wa ndani ya uwanja mpaka kufungwa kwa dirisha la usajili wa majira ya kiangazi juzi.
Golikipa, Petr Cech ndiye mchezaji pekee aliyesajiliwa kwa paundi milioni 10 kutokea Chelsea.
Ukweli unaonesha kuwa Arsenal ya Wenger ndio klabu kubwa katika ligi tano za Ulaya ((Premier, La Liga, Serie A, Bundesliga na Ligue 1) ambayo haijanunua mchezaji wa ndani.
Hata mabingwa wa Hispania, Barcelona ambao kwasasa wamefungiwa usajili, waliweza kununua wachezaji wawili wakubwa.
Walimsajili kiungo wa Uturuki, Arda Turan kutokea Atletico Madrid kwa paundi milioni 25 na kiungo wa Sevilla, Aleix Vidal kwa ada ya paundi milioni 12.5, ingawa wote hawatacheza mpaka 2016.
Kitendo cha Gunners kutosajili, kimewaudhi mashabiki waliokubuhu wa timu hiyo 'Arsenal Supporters Trust' ambao wamehitaji sera ya usajili ya Wenger ichunguzwe haraka.
Lakini Wenger ambaye jana usiku alikuwa Nyon, Uswisi kwenye mkutano wa 2015 wa makocha wa juu wa UEFA ambapo alikutana na mpinzani wake wa zamani Sir Alex Ferguson alisema:
"Nina furaha na uwekezaji nilioweka? ndiyo, kila muda.
"Mwaka uliopita, nilimnunua (Alexis) Sanchez, nilimnunua (Mesut) Ozil, nilimnunua Cech, nilimnunua Gabriel".
0 comments:
Post a Comment